Kinole Akiba sasa ipo Karibu Yako.
Kuna Akiba za lazima na Akiba za hiari
Akiba za lazima ni akiba ambayo kila mwanachama anatakiwa awe nayo hasa wakati wa kukopa, ambapo mwanachama atakopeshwa si zaidi ya mara tatu ya akiba alizoweka katika chama.
Akiba za hiari ni akiba ambazo mwanachama ataweka SACCOS kwaajili ya kulipwa faida, ambapo mwanachama akiweka akiba hizi atalipwa faida ya 5 – 6% kwa mwaka kutegemea na kiasi kitakachowekwa.
Kima cha chini cha kuweka akiba ni TZS 10,000 na kima cha juu ni uwezo wa mwanachama.